Posts

SOMO LA 100

SOMO LA 100: MATUMIZI YA "that's where" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ That's where = that is where ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. If you didn't know, that's where I live. 👉 Kama haukujua, hapo ndipo ninapoishi 2. That's where the problem begins. Never argue with an angry person 😡 Hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kamwe usibishane na mtu aliyekasirika 3. You will go to Asia and that's where you will spend your holiday with your family ✈ Utakwenda Asia na hapo ndipo utakapoitumia likizo yako na familia yako 4. My friend, that's where all the money is. Don't despise that opportunity 💰 Rafiki yangu, hapo ndipo pesa zote zilipo. Usiidharau fursa hiyo 5. I met Shukuru at his office because that's where he spends most of his time daily 🏢 Nulimkuta Shukuru ofisini kwake kwa sababu hapo ndipo anapoutumia muda wake mwingi kila siku 6. Is that where you want to reach in life? Don't give up. 💪 Je, hapo ndipo unapotaka kufika katika maisha?...

SOMO LA 99

SOMO LA 99: MATUMIZI YA "what" SEHEMU B: ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ Examples (mifano): 1. Stick to what you believe. Don't doubt your beliefs 👉 Ng'ang'ana kwenye unachokiamini. Usitilie shaka unavyoviamini (imani zako) 2. What I heard about you was not true. Today I have proved 👉 Nilichokisikia kuhusu wewe hakikuwa kweli. Leo nimethibitisha 3. What most people want in life is money and love 👉 Ambacho watu wengi wanataka katika maisha ni pesa na upendo 4. What I can say is this, you have to work hard 👉 Ninachoweza kusema ni hiki, unatakiwa kufanya kazi kwa bidii. 5. What I want to buy is not available in this boutique 👉 Ninachotaka kununua hakipo katika duka hili (la nguo) 6. Tell us what you want. We are ready to do it for you 👉Tuambie unachotaka. Tuko tayari kukifanya kwa ajili yako 7. I would like to know what you are thinking about this business 👉 Ningependa kujua ni nini uko unafikiria kuhusu biashara hii 8. In life you don't get what yo...

SOMO LA 98

SOMO LA 98: MATUMIZI YA "that's what" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ That's what = that is what ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. That's what I mean. There's nothing else 👉 Hicho ndicho ninachomaanisha. Hakuna kitu kingine chochote. 2. Yes, that's what I want from you. Thank you very much 👉 Ndiyo, hicho ndicho ninachokitaka kutoka kwako. Asante sana 3. Don't be afraid of smiling because that's what you should always do 👉  Usiogope kutabasamu kwa sababu hicho ndicho unachotakiwa kufanya mara zote 4. Don't put words in my mouth. That's not what I said please 👉 Usiweke maneno kinywani mwangu. Hicho sicho nilichosema tafadhali 5. Although that's what most people believe, the fact is that it's wrong 👉 Ingawa hicho ndicho watu wengi wanaamini ukweli ni kwamba si sahihi 6. Is that what you were thinking about? 👉 Je, hicho ndicho ulichokuwa unafikiria? 7. Is that what investors want to do for our country? 👉 Hicho ndicho wawekez...

SOMO LA 97

SOMO LA 97: MATUMIZI YA "whom" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. Whom do you want to live with? 👉 Unataka kuishi na nani? 2. Whom are you talking about? I just want to know 👉 Uko unamuongelea nani? Ninataka kujua tu 3. That's a nice house. By whom was that house built? 👉 Hiyo ni nyumba nzuri. Nyumba hiyo ilijengwa na nani? 4. To whom would you like to go? Do you have a bus fare? 👉 Ungependa kwenda kwa nani? Una nauli ya basi? 5. Whom were you welcoming? It was a party of its own kind 👉 Mlikuwa mko mnamkaribisha nani? Ilikuwa tafrija ya aina yake 6. Whom did you invite? When will he arrive here? 👉 Ulimualika nani? Atawasili hapa lini? 7. There are many preachers nowadays. Whom do you believe? 👉 Kuna wahubiri wengi siku hizi. Unamuamini nani? 8. Calm down. Whom are you looking for? 👉 Tulia. Uko unamtafuta nani? 9. Whom can we send to the chemist? We want to test the quality of this chemical 👉 Tunaweza kumtuma nani kwa mkemi...

SOMO LA 96

SOMO LA 96: MATUMIZI YA "whose" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ Examples (mifano): 1. Whose phone is this? I have found it under the bench 👉 Hii ni simu ya nani? Nimeikuta chini ya benchi 2. Whose problem is it? Is it mine or yours? 👉 Ni tatizo la nani? Ni langu au lako? 3. Whose grandmother did you go to the hospital to visit? 👉 Ni bibi wa nani ulikwenda kumuona (kumtembelea) hospitalini? 4. Whose case will it be if I don't clear this debt? 👉 Itakuwa kesi ya nani kama silipi deni hili? 5. Whose cheque are you taking to the bank? What does a cheque look like? 👉 Ni hundi ya nani uko unaipeleka benki? Hundi inafananaje? 6. Whose phone is ringing? Please, keep your phone in a vibration mode 👉 Ni simu ya nani (iko) inalia? Tafadhali, weka simu yako kwenye mtetemo 7. Whose relationship was broken by her sister in law? 👉 Ni mahusiano ya nani yalivunjwa na wifi yake? 8. If your mother gives you an advice and your best friend gives you a different advice, whose advic...

SOMO LA 95

SOMO LA 95: MATUMIZI YA "who" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ Doesn't = does not ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. Who are you? I am asking you 👉 Wewe  ni nani? (Niko) ninakuuliza wewe 2. Who is talking about things he doesn't know? I just want to know him 👉 Ni nani yuko anaongelea mambo asiyoyajua? Ninataka kumjua tu 3. Who is the head of this family? Tell him/her to come 👉 Nani ni mkuu wa familia hii? Mwambie aje 4. Who can save this child? She is facing a very great challenge. 👉 Ni nani anaweza kumuokoa mtoto huyu? Anakabiliana na changamoto kubwa sana 5. Who is who? Each of you claims to be the leader. It's confusing 👉 Nani ni nani? Kila mmoja wenu anadai kuwa ndiye kiongozi. Inachanganya 6. Who made it? Is it made in Tanzania? 👉 Ni nani aliyekitengeneza? Kimetengenezwa Tanzania? 7. Who can answer this question? If you know the right answer lift up your right hand 👉 Ni nani anaweza kujibu hili swali? Kama unajua jibu sahihi inua mkono wako wa kuli...

SOMO LA 94

SOMO LA 94: MATUMIZI YA "when" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. When will you bring my money? 👉 Utaleta pesa zangu lini? 2. When would you like to start your journey? 👉 Ungependa kuanza safari yako lini? 3. When did this happen? I don't know anything about this event 👉 Hili lilitokea lini? Sijui kitu chochote kuhusu tukio hili. 4. Your cake is ready. When will you come to collect it? 👉 Keki yako iko tayari. Utakuja kuichukua lini? 5. When will the president come to visit this village and witness what we are going through? 👉 Ni lini Rais atakuja kutembelea kijiji hiki na kushuhudia tuchokipitia? 6. You are grown up. When will you stop acting like a little child? 👉 Umekua. Ni lini utaacha kutenda kama mtoto mdogo? 7. I am sorry for any inconveniences. When will you increase my salary? 👉 Samahani kwa usumbufu wowote. Ni lini utauongeza mshahara wangu? 8. First, when were you born? Second, Where were you born? 👉 Kwanza, ulizaliw...

SOMO LA 93

SOMO LA 93: MATUMIZI YA "why" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. Why are you looking at me as if it's your first time to see me? 👉 Kwa nini uko unanitazama kama vile ni mara yako ya kwanza kuniona? 2. Why do you want to do so before you ask for permission? 👉 kwa nini unataka kufanya hivyo kabla haujaomba ruhusa? 3. Why did you sleep during the meeting? Were you sick? 👉 Kwa nini ulilala wakati wa mkutano? Ulikuwa unaumwa? 4. Why is it possible to watch TV for many hours but not possible to pray for many hours? 👉 Kwa nini inawezekana kutazama TV kwa saa nyingi lakini haiwezekani kuomba/kusali kwa saa nyingi? 5. Why is water more important than soda and other drinks? 👉 Kwa nini maji ni muhimu kuliko soda na vinywaji vingine? 6. Why is there no difference between these people although they have different backgrounds? 👉 Kwa nini hakuna tofauti kati ya watu hawa ingawa wana historia tofauti? 7. Why have you decided to quit that job? Have ...

SOMO LA 92

SOMO LA 92: MATUMIZI YA "which" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. Don't panic. Which boy are you looking for? 👉 Usihofu. Uko unamtafuta mvulana gani? 2. There are many cars here, which car would you like to buy? 👉 Kuna magari mengi hapa, ni gari lipi ungependa kununua? 3. Which kind of food would you like to eat today? 👉 Ni aina gani ya chakula ungependa kula leo? 4. Which TV channel are you watching? Are you aware of any movie or news  channels? 👉 Ni kituo kipi cha TV uko  unatazama? Unajua vituo vyovyote vya filamu au habari? 5. I have information about her sickness. To which hospital is she admitted? 👉 Ninataarifa kuhusu kuugua kwake. Amelazwa kwenye hospitali ipi? 6. Which country is the richest in the world? If you give the right answer I will prepare a gift for you 👉 Ni nchi ipi ni tajiri zaidi duniani? Kama unatoa jibu sahihi nitaanda zawadi kwa ajili yako. 7. Which disease are you suffering from? I see you at this hospital ...

SOMO LA 91

SOMO LA 91: MATUMIZI YA "how" ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖ ⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪⚪ Examples (mifano): 1. How  are you? How is your family? 👉 Hujambo? Familia yako haijambo? 2. How have you cooked this food? It is very delicious 👉 Umepikaje chakula hiki? Ni kitamu sana. 3. How can I help you? Do you have a bank account? 👉 Ninaweza kukusaidiaje? Una akaunti ya benki? 4. How will this be possible? I need your explanations please 👉 Hili litawezekanaje? Ninahitaji maelezo yako tafadhali 5. How did you get my phone number? If you don't tell me I will block your number and report you to the police 👉 Ulipataje namba yangu ya simu? Kama hauniambii nitaizuia namba yako na kukuripoti pilisi 6. Don't you give up? How many times would you like to repeat this exercise? 👉 Haukati tamaa? Ni Mara ngapi ungependa kurudia zoezi hili? 7. I am sorry. I am a stranger. How far is the ocean from the city centre? 👉 Samahani. Mimi ni mgeni. Bahari iko umbali gani kutoka katikati ya jiji? 8...