SOMO LA 99


SOMO LA 99: MATUMIZI YA "what"
SEHEMU B:
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Examples
(mifano):
1. Stick to what you believe. Don't doubt your beliefs
👉 Ng'ang'ana kwenye unachokiamini. Usitilie shaka unavyoviamini (imani zako)

2. What I heard about you was not true. Today I have proved
👉 Nilichokisikia kuhusu wewe hakikuwa kweli. Leo nimethibitisha

3. What most people want in life is money and love
👉 Ambacho watu wengi wanataka katika maisha ni pesa na upendo

4. What I can say is this, you have to work hard
👉 Ninachoweza kusema ni hiki, unatakiwa kufanya kazi kwa bidii.

5. What I want to buy is not available in this boutique
👉 Ninachotaka kununua hakipo katika duka hili (la nguo)

6. Tell us what you want. We are ready to do it for you
👉Tuambie unachotaka. Tuko tayari kukifanya kwa ajili yako

7. I would like to know what you are thinking about this business
👉 Ningependa kujua ni nini uko unafikiria kuhusu biashara hii

8. In life you don't get what you feel like having but what you are ready to work for
👉 Katika maisha haupati ambacho unajisikia kuwa nacho bali ambacho uko tayari kukifanyia kazi

9. I can't own something like that. What I want to own is very different from what you think
👉 Siwezi kumiliki kitu kama  hicho. Ninachotaka kumiliki ni tafuauti sana na kile unachofikiria

10. I mean what I say and I say what I mean
👉 Ninamaanisha ninachokisema na ninasema ninachokimaamisha ➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌐 Facebook/Instagram/YouTube @ Azari Eliakim  

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA 110

SOMO LA 1

SOMO LA 2