SOMO LA 110


SOMO LA 110: MATUMIZI YA "that's when"
SEHEMU B:
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Examples
(mifano):
6. Is that when you will start the journey? Whom will you travel with? I would like to escort you to the bus station
👉 Wakati huo ndipo utaanza safari? Utasafiri na nani? Ningependa kukusindikiza kwenye kituo cha basi

7. Is that when you sent me this message? I have seen it just now. I am very sorry for letting you down. I didn't intend to disappoint you
👉 Wakati huo ndipo uliponitumia ujumbe huu? Nimeuona sasa hivi tu. Ninasikitika sana kwa kukuangusha. Sikukusudia kukufedhehesha

8. Is that when you will come? Try to come as early as possible because I might not be around for a couple of days.
I might be on a business trip
👉 Wakati huo ndipo utakapokuja? Jaribu kuja mapema iwezekanavyo kwa sababu yawezekana nisiwepo kwa siku kadhaa. Ninaweza kuwa kwenye safari ya kibiashara

9. I saw you at the hospital yesterday morning. Is that when you were going for a diagnosis?
👉 Nilikuona hospitalini jana asubuhi. Wakati huo ndipo ulipokuwa unakwenda kwa ajili ya uchunguzi (vipimo)?

10. Is that when I have to be at the airport? I will miss my morning sleep. I wish I had the authority of changing this flight schedule
👉 Wakati ndipo ninatakiwa kuwa kwenye uwanja wa ndege? Nitaukosa usingizi wangu wa asubuhi. Ninatamani ningekuwa na mamlaka ya kubadilisha hii ratiba ya kupaa
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌐 Facebook/Instagram/YouTube @ Azari Eliakim  

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA 1

SOMO LA 93