SOMO LA 83
SOMO LA 83: MATUMIZI YA "would like"
SEHEMU A:
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Examples
(mifano):
1. I would like to begin with you
👉 Ningependa kuanza na wewe
2. I would like to know your name please
👉 Ningependa kujua jina lako tafadhali
3. I would like to introduce my family to you
👉 Ningependa kuitambulisha familia yangu kwako/kwenu
4. My child would like to play with his/her fellow kids
👉 Mwanangu angependa kucheza na watoto wenzake
5. I would like to tell you the secret of my life but make sure that you keep it
👉 Ningependa kukwambia siri ya maisha yangu lakini hakikisha kwamba unaitunza
6. I would not like to see you suffering again
👉 Nisingependa kukuona ukiteseka (ukisumbuka) tena
7. I would like to have a cup of tea before I go to bed
👉 Ningependa kupata kikombe cha chai kabla sijakwenda kitandani
8. I would like to help you because I want you to be successful
👉 Ningependa kukusaidia kwa kuwa ninataka wewe ufanikiwe
9. If you didn't know, let me tell you. You are a unique person and I would like you to believe so
👉 Kama haukujua, ngoja nikwambie. Wewe ni mtu wa kipekee na ningependa wewe uamini hivyo
10. We have nothing to do, so we would like you to tell us what to do
👉 Hatuna kitu chochote cha kufanya, hivyo tungependa wewe utwambie (nyinyi mtwambie) nini cha kufanya
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌐 Facebook/Instagram/YouTube @ Azari Eliakim
Comments