SOMO LA 108
SOMO LA 108: MATUMIZI YA "why"
SEHEMU B:
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Examples
(mifano):
1. I don't understand why this is happening to me
👉 Sielewi kwa nini hili linanitokea
2. If you want to know why this is happening to you ask your mentor
👉 Kama unataka kujua kwa nini hili linakutokea muulize mshauri wako
3. You have to be aware of what you want and why you want it
👉 Unatakiwa kujua unachokitaka na kwa nini unakitaka
4. Let's just wait, the teacher will tell us why he doesn't want to teach us at night
👉 Hebu tusubiri tu, mwalimu atatwambia kwa nini hataki kutufundisha usiku
5. You never know. Maybe she knows why this is not going to happen
👉 Huwezi jua. Labda anajua kwa nini hili halitatokea
6. I saw the number on the advert but I don't know why I didn't write it somewhere
👉 Niliiona namba kwenye tangazo lakini sijui kwa nini sikuiandika mahali fulani
7. Most citizens want to be told why it's not raining while it's a rainy season
👉 Wananchi wengi wanataka kuambiwa kwa nini mvua hainyeshi wakati ni msimu wa mvua
8. I don't know why you are accusing me of something I have not done
👉 Sijui kwa nini unanishutumu kwa kitu ambacho sijakifanya
9. I don't agree with you. That's not a good reason why you shouldn't come
👉 Sikubaliani na wewe. Hiyo si sababu nzuri kwa nini hautakiwi kuja
10. Hold on. There is no reason why you can't succeed
👉 Subiri kidogo. Hakuna sababu kwa nini hauwezi kufanikiwa
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌐 Facebook/Instagram/YouTube @ Azari Eliakim
Comments
https://adultvideos.ml