SOMO LA 107
SOMO LA 107: MATUMIZI YA "that's why"
SEHEMU B:
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Examples
(mifano):
6. I have never seen something like this in my entire life that's why it's very hard to believe whether it's real or not
👉 Sijawahi kuona kitu kama hiki katika maisha yangu yote ndiyo sababu ni vigumu kuamini kama ni halisi au la
7. Is that why you are angry with me? I was just kidding, I didn't mean to hurt you so just forgive me. I won't do it again, I promise you
👉 Hiyo ndiyo sababu umenikasirikia? Nilikuwa niko ninatania tu, sikumaanisha kukuumiza hivyo nisamehe tu.
Sitalifanya tena, ninakuahidi
8. Is that why you want to revenge? Vengeance is useless because it will open doors for more problems instead of joy. I beg you, don't revenge. Let God stand for you
👉 Hiyo ndiyo sababu unataka kulipa kisasi? Kisasi hakifai kwa sababu kitafungua milango kwa ajili ya matatizo zaidi badala ya furaha. Ninakuomba, usilipe kisasi. Acha Mungu asimame kwa ajili yako
9. Oh my God, doctor is that why I have lost my friend? I really don't understand how malaria can lead to such a sudden death.
👉 Ee Mungu wangu, daktari hiyo ndiyo sababu nimempoteza rafiki yangu?
Hakika sielewi jinsi ambavyo malaria inaweza kusababisha kifo cha ghafla namna hii
10. Becoming a billionaire is not as easy as you think that's why billionaires are countable.
👉 Kuwa bilionea si rahisi kama unavyofikiria ndiyo sababu mabilionea wanahesabika
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌐 Facebook/Instagram/YouTube @ Azari Eliakim
Comments