SOMO LA 104
SOMO LA 104: MATUMIZI YA "how"
SEHEMU B:
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Examples
(mifano):
1. If you know how to write a job application letter please teach me
👉 Kama unajua jinsi ya kuandika barua ya kuomba kazi tafadhali nifundishe
2. My mother has a lot of money but she doesn't know how to spend it properly
👉 Mama yangu ana pesa nyingi sana lakini hajui jinsi ya kuzitumia kwa usahihi
3. I want to learn how to speak and write English well
👉 Ninataka kujifunza jinsi ya kuongea na kuandika kiingereza vizuri
4. This shows how intelligent you are. Most people fail this exam
👉 Hii inaonyesha jinsi ulivyo na akili. Watu wengi huwa wanashindwa mtihani huu
5. I just feel like there is something wrong with me because how you look at me scares me
👉 Ninahisi tu kama kuna kitu fulani hakiko sawa kwangu kwa sababu unavyonitazama inanitisha
6. I understand how you are feeling now. What you are going through is tough
👉 Ninaelewa vile ambavyo uko unajisikia sasa. Unalolipitia ni gumu
7. There is a very big difference between between how people treat rich friends and how they treat poor friends
👉 Kuna tofauti kubwa sana kati ya jinsi ambavyo watu wanawachukulia marafiki tajiri na jinsi wanavyowachukulia marafiki masikini
8. Life is how you make it. Be responsible and take care of your life.
👉 Maisha ni vile unavyoyatengeneza.
Wajibika na kuwa makini na maisha yako.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌐 Facebook/Instagram/YouTube @ Azari Eliakim
Comments