SOMO LA 103
SOMO LA 103: MATUMIZI YA "that's how"
SEHEMU B:
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Examples
(mifano):
6. I am not afraid of any wild animal. That's how confident I am.
👉 Simuogopi mnyama yeyote wa porini. Hivyo ndivyo nilivyo jasiri
7. When you start taking a glass of alcohol watch out because that's how drunkenness begins
👉 Unapoanza kunywa glasi ya pombe kuwa makini kwa kuwa hivyo ndivyo ulevi unavyoanza
8. Because they are identical twins I will ask them tricky questions and that's how I will know who is who
👉 Kwa sababu ni mapacha wanaofanana nitawauliza maswali ya mitego na hivyo ndivyo nitajua yupi ni yupi
9. That's how most people use their cell phones. They don't care about the privacy of other cell phone users
👉 Hivyo ndivyo watu wengi wanavyotumia simu zao za mkononi. Hawajali usiri wa watumiaji wengine wa simu za mkononi
10. Is that how you want me to live? I am sorry, it won't be possible. Live your life and let me live my own life
👉 Hivyo ndivyo unavyotaka mimi niishi? ninasikitika, haitawezekana.
Ishi maisha yako na niache mimi niishi maisha yangu mwenyewe
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌐 Facebook/Instagram/YouTube @ Azari Eliakim
Comments